Wanahisa
Benki ya Access Microfinance Tanzania inamilikiwa na wanahisa watano wanaotambulika kimataifa.

Access Microfinance Holding AG (AccessHolding)
Access Holding ni kampuni mama simamizi ya Access Group, mtandao wa benki za biashara unao lenga biashara za chini, ndogo, ndogo na za kati. Kundi hili kwa sasa linajumuisha benki wanachama nane katika kanda mbalimbali za dunia, sita kati yao ziko Kusini mwa Jangwa la Sahara (na Benki ya Access Microfinance Tanzania ikiwa kubwa zaidi). Kwa jumla ya mali inayozidi dola bilioni 1.2 na zaidi ya wateja 800,000 (hadi tarehe 31 Desemba 2013), Access Group ni mojawapo ya mitandao ya benki inayoongoza ya mikopo midogo midogo duniani kote.
International Finance Corporation (IFC)
Ni tawi la sekta binafsi la Benki ya Dunia ambalo hutengeneza fursa kwa watu kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao. IFC inakuza ukuaji endelevu wa uchumi katika nchi zinazoendelea kwa kusaidia maendeleo ya sekta binafsi huku ikikusanya mtaji wa kibinafsi.

Micro Vest
Micro Vest ni kikundi cha kibinafsi cha uwekezaji kwa faida kilichojikita kupunguza umaskini duniani kwa kutumia mfumo wa kibiashara kwenye uwekezaji.

KfW – The German Development Bank
KfW ni benki ya maendeleo ya Ujerumani, sehemu muhimu ya KfW Bankengruppe na chini ya umiliki wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani na majimbo yake ya Shirikisho. Taasisi hufadhili, kushauri na kusaidia miradi na programu za maendeleo kote ulimwenguni.
African Development Bank (AfDB)
Benki ya Maendeleo ya Afrika ni taasisi ya kikanda ya kimataifa ya kifedha ya maendeleo ambayo ilianzishwa ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya kijamii ya nchi na wanachama wake.
Benki ya Access Microfinance Tanzania imejaliwa kuwa na mtaji wa shilingi bilioni 40 ukigawanywa katika hisa milioni 40 ambazo kwa sasa zinagawanywa kama ifuatavyo;
Wanahisa |
% |
AccessHolding |
66.11% |
IFC |
13.06% |
MicroVest |
9.04% |
KfW |
6.73% |
AfDB |
5.06% |
Jumla ya Hisa |
100.00% |