Je, ungependa kutuma pesa kwa mtu aliye hapa hapa nchini au mtu anayeishi nje ya nchi au unatarajia kupokea pesa kutoka ng’ambo? Uhamisho wa pesa wa kimataifa unapatikana katika tawi lolote la Access Microfinance. Benki ya Access Microfinance inatoa aina zifuatazo za uhamisho wa pesa;

Uhamishaji wa pesa ndani ya mtandao wa tawi la Benki ya Access Microfinance

 

Hakuna ada zitakazotozwa kwa uhamisho wa pesa kati ya akaunti ndani ya mtandao wa tawi la Benki ya Access. Kwa kuwa matawi yetu yote yameunganishwa kupitia mfumo wa kidigitali, malipo hufanyika kwa uharaka sana!

Kuhamisha pesa ndani na nje ya nchi

 

Tunatoa Uhamisho wa pesa za Kitaifa kwa benki zote ndani ya Tanzania kwa ada isiyobadilika ya shilingi 10,000 kwa uhamisho bila kujali kiasi gani. Uhamisho kwa Dola ya Marekani au uhamisho nje ya nchi kupitia mfumo wa SWIFT huvutia gharama za juu zaidi. Tafadhali wasiliana na tawi lako la karibu kwa maelezo zaidi.