Akaunti ya KIKUNDI inawezeshwa na AccessMobile

”Usalama na Ukaribu zaidi wa fedha Zako”

Akaunti ya akiba ambayo imeundwa mahususi kwa ajili ya vikundi vya Akiba, Vyama vya Mikopo (VSLA), VICOBA, SACCOS au vikundi vinavyojulikana zaidi kama vikundi visivyo rasmi vya kuweka akiba. Bidhaa hiyo inatoa fursa au ‘jukwaa’ kwa vikundi kuhusu jinsi ya kusimamia fedha zao ‘kidigitali’. Akaunti hii ina mfumo 3 wa benki kwa njia ya simu unaohakikisha kiwango cha juu zaidi cha usalama wa kiwango cha benki na vile vile vikundi na wanachama wao kuweza kujivinjari kwa kufanya miamala wakiwa mbali. Jukwaa hili huwezesha vikundi kuendelea na biashara zao za kila siku bila kuharibu uhusiano na tabia zao za kijamii”.

Faida Ya Akaunti

  • 1. Kiwango cha kufungua akaunti shilingi 10,000
  • 2. Kupata huduma kwa njia ya simu mobile banking (AccessMobile) ikiwemo kuhamisha pesa kutoka benki kwenda kwenye simu.
  • 3. Kiwango cha riba cha kuvutia cha hadi 4%,
  • 4. Uwezeshaji/kufungua akaunti papo hapo katika matawi.
  • 5. Kuweka pesa ni bure katika (matawi, mobile banking, na wakala).
  • 6. Kitabu cha kutoa pesa ya kikundi kinatolewa.
  • 7. Kutoa pesa kwa WAKALA yeyote wa Access nchi nzima.