Kuunganishwa wa matawi ya Mkunguni na Lumumba yaliyopo Kariakoo – Dar es Salaam

Wapendwa wateja, Awali ya yote, Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa AccessBank Tanzania inawatakia heri ya mwaka mpya 2020 na kuwashukuru sana kwa kuendelea kutumia huduma zetu vizuri.  Kutokana na maboresho na kuimarika kwa njia mbadala za utoaji wa huduma za kibenki kwa sasa,na ukaribu uliopo wa matawi yetu mawili ndani ya eneo la Kariakoo, (umbali usiozidi kilomita moja), tunapenda kuwataarifu kuwa  tawi la Mkunguni lililopo mtaa wa Mkunguni litaunganishwa na tawi la Lumumba lililopo mtaa wa Lumumba na Kipata…