Benki ya Access Microfinance inatoa mikopo ya Kilimo kwa mkulima mmoja mmoja kuanzia shilingi 500,000/- hadi Shilingi 50, 000,000/- yenye lengo la kutoa msaada wa kifedha wa kutosha na kwa wakati kwa wakulima ili kuimarisha shughuli zao za kilimo (Pembejeo, Kazi, Vifaa vya Shamba, Uwekezaji nk.)

Mchakato wa Mkopo wa Kilimo

 

  1. 1. Ukaguzi/Maombi katika tawi au kijiji
  2. 2. Wawakilishi kutoka benki watakutembelea kuzungumzia kilimo na mpango wako kama mteja
  3. 3. Kutembelea mashamba, nyumba na mifugo
  4. 4. Kamati ya mikopo; Uamuzi wa ukomavu wa kiasi cha mkopo (miezi 3 hadi 12) na mpango wa ulipaji.
  5. 5. Kusaini mkataba na malipo
  6. 6. Marejesho kwenye tawi kupitia simu au wakala wa benki.

 

Faida

 

  • Mchakato wa haraka sana: Siku 3 kupata mkopo wako!
  • Mpango wa ulipaji unaobadilika kulingana na shughuli za kilimo binafsi na mtiririko wa pesa wa kila mwezi
  • Hakuna haja ya kuwa na akaunti katika benki
  • Uwazi wa hali ya juu na hakuna rushwa

 

Vigezo na Masharti

 

    • 1. Mahitaji: Mtanzania mwenye umri zaidi ya miaka 18 na tayari ni mkulima
    • 2.Nyaraka zinazohitajika: Moja kati ya kitambulisho cha kupiga kura, pasipoti, leseni ya udereva, mwenyekiti/barua ya kata + leseni ya biashara (ikiwa una biashara)
    • 3. Dhamana: mifugo, vitu vya nyumbani na biashara, nyumba, mashamba, magari..

 

Matawi Yetu (Kupata Mkopo wa Kilimo)

 

    • 1. Mwanza: Kituo cha Biashara cha Pamba cha wafanyabiashara wadogo (SME) kando ya Barabara ya Pamba, jengo la Kishimba Kiwanja Na.140
    • 2. Tawi la Kahama: Barabara ya Isaka, Majengo
    • 3. Tawi la Tabora: Barabara ya Isikie, Jengo la NSSF
    • 4. Tawi la Mbeya: Mafiati, mkabala na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)