Mikopo ya Biashara Midogo Na Saizi Ya Kati (SME)

 

Mikopo ya wafanyabiashara wadogo na saizi ya kati (SME) kuanzia Shilingi 35,000,001 na kuendelea. Hakuna kikomo cha juu kilichobainishwa cha kiasi cha mkopo kwani kiwango na muda wa kulipa mkopo huo hutegemea sana nguvu na uwezo wa kulipa deni wa biashara yako.

Faida shindani za mkopo kwa Wafanyabiashara Wadogo na Saizi ya Kati (SME)

 

  • 1. Mipangilio mzuri wa dhamana kulingana na kiwango cha mkopo (bidhaa za nyumbani, vifaa vya biashara, bidhaa kwenye hisa, magari, mali isiyohamishika n.k.)
  • 2. Nyaraka zinazohitajika ni chache ukilinganisha na benki nyingine katika soko la biashara. Hakuna taarifa za fedha zilizokaguliwa zinazohitajika.
  • 3. Huhitaji kuwa na uhusiano wa awali na Benki ya Access Microfinance. Huhitaji kuwa umetumia akaunti ya Benki ya Access Microfinance kwa muda wowote kabla ya kutuma ombi. Hata hivyo ni faida ikiwa unaweza kuonyesha uzoefu wowote wa awali wa kukopa au benki.
  • 4. Hakuna usiri wa gharama kama vile ada na kamisheni za ziada: Maafisa wetu wa mikopo watafurahi kukusaidia kwa kulinganisha viwango vya riba.
  • 5. Wateja wa muda mrefu walio na rekodi ya kuvutia ya urejeshaji wataweza kupata punguzo la viwango vya riba mfululizo na pia wataweza kupata mikopo kwa haraka.
  • 6. Hakuna vikundi vya wakopaji – unawajibika tu kwa mkopo wako mwenyewe.

 

Huduma ya Kukopa zaidi ya kiasi kilichopo (Over draft) kwa Wafanyabiashara wadogo na saizi ya kati (SME)

 

Wateja walengwa: wamiliki wa biashara zisizo rasmi ambao wanaendesha akaunti zao hai na Benki ya Access Microfinance Tanzania kwa angalau miezi mitatu na kutoka Benki nyingine kwa angalau mwaka mmoja.

Lengo: Kwa matumizi ya biashara ya muda mfupi yanayohitaji pesa kwa shughuli za kawaida, hakuna madhumuni yoyote ambayo yamekatazwa na Orodha ya iliyopo inayotolewa na Sera ya Mikopo.

Kiwango cha chini; kiasi cha mkopo wa Over Draft kisiwe chini ya shilingi milioni ≤ 15,000,00.

Kiwango cha juu: shilingi milioni 500,000,000 kwa wateja wapya ambao wana miamala mizuri kutoka taasisi nyingine za fedha.