Dhamira Ya Benki
Benki ya Access Microfinance ni benki inayowajibika kijamii kwa tabaka la watu wa kipato cha chini na cha kati katika jamii ya Kitanzania. Ni benki chaguo namba moja kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Inafanya kazi kwa juhudi kubwa ili iweze kufikia kuwa mtoaji mkuu wa huduma za kifedha nchini Tanzania
Benki ya Access Microfinance imejenga uhusiano wa muda mrefu wa biashara na mteja ikilenga hasa katika uwajibikaji na uelewano wa pamoja. Kwa kufanya hivyo ilikuza utamaduni wa kuweka akiba, kutoa huduma ya malipo na akaunti na kusaidia wakopaji kuweka historia ya mkopo. Mikopo ya benki kimsingi inategemea tathmini ya uwezo wa ulipaji wa mkopaji.
Maono Ya Benki
Ni Kujidhatiti katika uanzishaji wa mifumo ya kifedha inayochochea maendeleo ya jamii kwa kutoa huduma zilizobora kwa watu wote.